Michezo ya mwaka 2024 ya Olimpiki imefungwa wiki iliyopita huko Paris, Ufaransa. Tovuti ya maoni ya kisiasa ya Australia “Lulu na Misisimko” hivi majuzi imetoa makala ya uchambuzi ikisema wakati wa Michezo hiyo, Marekani ilitoa madai yasiyo na ukweli dhidi ya China katika suala la matumizi ya dawa ya kusisimua misuli, lakini ukweli ni kwamba, Marekani ndio nchi ambayo haikuwa mkweli katika michezo hiyo ya Olimpiki.
Tovuti ya “Lulu na Misisimko” ni jukwaa la mtandaoni la Australia linalojadili sera za umma za ndani na kimataifa lililoanzishwa na ofisa mwandamizi wa zamani wa Baraza la Mawaziri la Australia, na waandishi wengi wa tovuti hiyo ni wanasiasa maarufu wa nchi hiyo akiwemo Waziri Mkuu za zamani Paul Keating.
Wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris, Marekani ilifanya njama kwa kisingizio cha kesi isiyo na msingi iliyotokea miaka mitatu iliyopita ili kuvuruga maandalizi ya timu ya China. Chini ya shinikizo la Marekani, Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua misuli (WADA) lilitekeleza ukaguzi wa dawa hizo unaoweza kuitwa kuwa mkali zaidi katika historia, lakini halikugundua shida lolote. Hata hivyo, Marekani iliendelea kusumbua na kudai WADA siyo mwaminifu, ama halina uwezo wa kufanya kazi vizuri. WADA lilikanusha tamko hilo na kukosoa Marekani kwa kuingiza mambo ya kisiasa katika michezo.
Marekani ilijaribu kutumia suala la dawa za kusisimua misuli kama silaha ya kushinda China. Hata hivyo, timu ya China ilijishindia medali nyingi, ikiwa na jumla ya medali 40 za dhahabu, na kufungana na Marekani kwa nafasi ya kwanza kwenye orodha ya medali za dhahabu za michezo ya Olimpiki ya Paris, huku Hong Kong na Taiwan kila moja ikishinda medali mbili za dhahabu. Hivyo idadi ya jumla ya medali za dhahabu zilizopatikana na China imepita Marekani.
Jambo lingine lisilotarajiwa na Marekani ni kwamba siri ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli ya wanariadha wake imefichuliwa.
Mwanariadha wa Marekani Erriyon Knighton aligunduliwa kutumia dawa za kusisimua misuli miezi 4 iliyopita. Kwa mujibu wa sheria za WADA, alipaswa kuzuiwa kushiriki kwenye michezo kwa angalau miaka minne. Hata hivyo, alishiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Paris na kukimbia muda wa sekunde 19.99 katika mchuano wa mita 200 kwa wanaume, vyombo vya habari viliuita mchuano huo ni “mchezo usio wa haki zaidi”.
Aidha, kulingana na utafiti wa vyombo vya habari, wanariadha wengi wa timu ya michezo ya Olimpiki ya Marekani wanaweza kutumia dawa zinazopigwa marufuku kihalali. Kwani kwa mujibu wa kanuni ya kimataifa ya michezo, wanariadha wenye magonjwa ya kupumua, moyo na mengineyo wanaweza kutumia dawa wakati wa michezo. Marekani imechukua fursa hii, na kudai wanariadha wake wengi hodari wana magonjwa hayo ili kutumia dawa zinazopigwa marufuku. “Je, inawezekana kuwatuma watu wengi wenye magonjwa hatari kwenye michezo ya ngazi ya juu zaidi duniani?” makala hiyo iliuliza.
Zaidi ya hayo, wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Paris, ilifichuliwa kuwa Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua Misuli la Marekani USADA liliwaruhusu wanariadha waliotumia dawa za kupigwa marufuku kutopata adhabu yoyote wakigundua na kuthibitisha wengine kutumia dawa hizo. Kitendo hicho kinakiuka kauni ya WADA na kulaumiwa vikali na jamii ya kimataifa.