Idara ya Afya ya Palestina kwenye Ukanda wa Gaza jana ilitoa taarifa ikisema, tangu mwezi Oktoba mwaka jana mgogoro kati ya Palestina na Israel ulipoanza, operesheni ya kijeshi ya Israel imesababisha vifo vya watu 40,005, na wengine 92,401 kujeruhiwa.
Taarifa hiyo pia imesema, katika saa 24 zilizopita, operesheni ya kijeshi ya Israel katika Ukanda wa Gaza imesababisha vifo vya watu 40, na wengine 107 kujeruhiwa.