Watu 54 wamefariki katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo la Tibesti kaskazini magharibi mwa Chad.
Kwa mujibu wa taarifa za nchi hiyo, mvua imeendelea kunyesha tangu tarehe 9 na kusababisha hasara kubwa kwa watu na miundombinu.
Wizara ya shughuli za kijamii, mshikamano wa kitaifa na masuala ya kibinadamu nchini humo imesema, serikali imefanya mkutano wa dharura kuhusu janga hilo na kuandaa mpango wa msaada.