Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Geng Shuang ametoa wito tena kwa kundi la Houthi la Yemen kuheshimu haki ya usafiri wa meli za biashara za nchi mbalimbali kwa kufuata sheria za kimataifa katika eneo la Bahari Nyekundu, kuacha vitendo vya usumbufu, na kulinda usalama wa njia ya meli katika eneo hilo.
Balozi Geng amesema, China inakaribisha makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya serikali ya Yemen na kundi la Houthi kuhusu masuala ya fedha na usafiri wa anga, pia inatarajia kuwa pande zote zinazohusika zitaendelea na juhudi kama hizo na kuondoa migogoro kwa njia ya mazungumzo.
Pia amesisitiza kuwa China inatoa wito kwa pande zote zinazohusika kujizuia na kuacha vitendo vya kuongeza hali ya wasiwasi kaitka eneo hilo.