"Soko la China limejaa uhai, pia serikali inapanua mahitaji ya ndani na kufanya mageuzi ya maendeleo yanayohifadhi mazingira, hali hii imetupatia nafasi nyingi za maendeleo. " naibu meneja mkuu wa kampuni ya Tesla Tao Lin alisema hayo baada ya afisa wa China kutangaza hali ya uendeshaji wa uchumi wa China tarehe Julai 15.
Kampuni ya Ujerumani ya sayansi ya maisha ya Bayer ilisema kwamba inatarajia kuwekeza euro milioni 20 ili kuanzisha kituo cha uvumbuzi mjini Shanghai mwaka huu.
Wakati huo huo, gaezeti la Ufaransa la "Le Figaro" lilisema kwamba wazalishaji wa Ujerumani wanatumai kupanua uzalishaji nchini China ili kutetea sehemu yao sokoni, na makampuni ya Ujerumani yanawekeza zaidi nchini China kuliko hapo awali.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu, makampuni ya kigeni yameendelea kuongeza uwekezaji nchini China, na hii ni "kura yao ya imani" kuhusu uchumi wa China. Watengenezaji wa mashine za plastiki za Ujerumani Arburg waliamua kuanza uzalishaji nchini China mwezi Agosti. Kampuni ya ABB Electric ya Uswisi, na mradi wa petroli wa Dayawan ya kampuni ya ExxonMobil ya Marekani wote wametangaza kuongeza mitaji nchini China. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kukuza Biashara ya Kimataifa la China inaonyesha kuwa zaidi ya 40% ya makampuni ya kigeni yaliyohojiwa yanaamini kuwa mvuto wa soko la China "unaongezeka." Licha ya mabadiliko ya hali ya kimataifa, China bado ni mahali pazuri kwa uwekezaji unaovutia umakini wa kimataifa.