Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema China na Russia ni kati ya vipaumbele vya sera za kigeni
2024-08-19 09:00:05| CRI

Waziri mteule wa mambo ya nje wa Iran Bw. Abbas Araghchi amebainisha vipaumbele vya sera za kigeni za nchi hiyo na kusisitiza umuhimu wa China na Russia.

Amesema China, Russia na nchi ambazo zimeiunga mkono Iran wakati ikikabiliwa na vikwazo, pamoja na nchi zinazoibuka za Afrika, Amerika ya Kusini na Asia Mashariki zitakuwa muhimu kwa sera ya mambo ya nje ya Iran. Pia amejitolea kuimarisha uhusiano na nchi jirani na kuunganisha miundombinu ya Iran na ya nchi hizo.

Amesema uhusiano na Ulaya unategemea kama Ulaya itabadilisha msimamo usio sahihi na wa uhasama dhidi ya Iran, na kuhusu uhusiano na Marekani amesisitiza mkakati wa kudhibiti uhasama wakati wa kufanya juhudi za kupunguza vikwazo.