Serikali ya Sudan kutuma wajumbe mjini Cairo kuhudhuria mazungumzo kuhusu makubaliano ya Jeddah
2024-08-19 08:53:14| CRI

Baraza la utawala wa mpito la Sudan limesema kuwa serikali ya Sudan itatuma wajumbe mjini Cairo, kuhudhuria mazungumzo ya kutekeleza makubaliano ya Jeddah yaliyosainiwa mwezi Mei mwaka 2023.

Baraza hilo limesema katika taarifa yake kuwa kwa mujibu wa mawasiliano na serikali ya Marekani, yaliyowasilishwa na mjumbe maalum wa Marekani kuhusu Sudan Bw. Tom Perriello, serikali ya Misri iliomba kufanya mkutano huko Cairo kujadili maoni ya serikali juu ya utekelezaji wa makubaliano ya Jeddah, na serikali itatuma wajumbe mjini Cairo.

Tarehe 14 Agosti mazungumzo ya amani yanayoongozwa na Marekani kuhusu mgogoro wa Sudan yalianza mjini Geneva, yakilenga kutimiza usitishaji vita kwa pande zote na kuhimiza upatikanaji wa misaada ya kibinadamu.