Hamas yakosoa pendekezo jipya la kusitisha mapigano Gaza kupendelea masharti ya Netanyahu
2024-08-19 08:54:07| CRI

Kundi la Hamas limekosoa pendekezo jipya la kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza lililotolewa huko Doha wiki iliyopita, kwa kupendelea masharti ya Waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamin Netanyahu hasa kukataa usitishwaji wa  kudumu wa mapambano .

Kundi hilo limetangaza kuwa pendekezo hilo linaendana na matakwa ya Netanyahu, ikiwemo kukataa makubaliano ya usitishwaji wa kudumu wa mapigano, kudumisha udhibiti wa Ukanda wa Netzarim, kivuko cha Rafah na Ukanda wa Philadelphi, na kuweka masharti mapya kuhusu mabadilishano ya wafungwa, huku likiongeza kuwa yote hayo yamezuia kukamilika kwa makubaliano.

Kundi la Hamas limemlaumu Netanyahu kuwajibika kikamilifu na kushindwa kwa wapatanishaji, kuzuia kufikiwa kwa  makubaliano na kuhatarisha usalama wa wafungwa wa Israel kwa kuendelea kufanya uvamizi dhidi ya Gaza.