Tanzania kupata kituo cha kwanza cha Akili Bandia (AI)
2024-08-19 23:21:58| cri

Tanzania inatazamiwa kupiga hatua kubwa katika teknolojia kwa ujenzi wa kituo chake cha kwanza cha Akili Bandia (AI) na kituo cha kuhifadhia taarifa za Roboti.

Mradi huo, utakaofadhiliwa na Benki ya Kiarabu ya Maendeleo ya Kiuchumi barani Afrika (BADEA), kwa sasa uko katika hatua za mipango, ikiashiria wakati muhimu kwa hali ya kidijitali nchini humo.

Taarifa ya ufadhili huo ilitolewa na Rais wa BADEA, Dk Sidi Ould Tah wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, kando ya kikao cha Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kilichofanyika mjini Harare, Zimbabwe.

Ingawa kutangazwa kwa kituo hicho ni hatua muhimu kwa matarajio ya kidijitali ya Tanzania, lakini maelezo mahususi kuhusu mradi huo bado hayajabainishwa.