Zambia yajitahidi kufufua sekta ya madini
2024-08-20 08:22:51| CRI

Waziri wa Madini wa Zambia Bw. Paul Kabuswe amesema mipango ya kufufua sekta ya madini imeanza kuzaa matunda na sekta hiyo sasa imefufuka.

Akiongea kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la Zambia, Bw. Kabuswe amesema uchumi mzima wa Zambia uliathirika kutokana na kuporomoka kwa sekta ya madini, ambayo ni mchangiaji mkuu  wa shughuli za kiuchumi.

Waziri huyo amesema, kufufuka kwa sekta ya madini kunatokana na hatua mbalimbali za uingiliaji zilizochukuliwa na Serikali katika miaka miwili iliyopita. Kwa sasa kampuni kubwa za madini zilizopanga kuondoka nchini Zambia zimeanza kuwekeza tena nchini humo, na kuleta mustakbali mzuri kwenye sekta hiyo.