Bara la Afrika linakabiliwa na ongezeko la ugonjwa wa maambukizi ya mbu, ikiwa ni pamoja na malaria na homa ya dengue, ambayo inaweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya ya umma, wanasayansi walionya Jumatatu wakati wa kongamano la mtandaoni lililofanyika kabla ya Siku ya Mbu Duniani .
Michael Charles, afisa mtendaji mkuu wa Shirika la Kutokomeza Malaria alisema, mabadiliko ya hali ya hewa yanachochea kuenea kwa mbu wanaohusika na maambukizi ya malaria na homa ya dengue barani Afrika, na kuathiri vibaya ukuaji wa uchumi.