Bodi ya Utalii ya Kenya (KTB) imesema mapato yanayotokana na sekta ya utalii ya nchi hiyo yamefikia shilingi bilioni 142.5 za Kenya (takriban dola za kimarekani bilioni 1.11) katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ambayo yamechangiwa na ongezeko kubwa la idadi ya watalii, ambapo idadi ya watalii wa kimataifa imeongezeka kwa asilimia 21.3 na kufikia milioni 1.03 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo huku ongezeko la idadi ya watalii wa ndani pia likishuhudiwa.
Ofisa mtendaji mkuu wa bodi hiyo June Chepkemei amesema ukuaji huo wa sekta ya utalii unatokana na juhudi za pamoja katika kuhimiza shughuli za utalii za maendeleo endelevu na kuboresha uzoefu wa watalii.
Habari nyingine zinasema Shirika la Ndege la Kenya limeripoti faida ya kwanza katika miaka 11 iliyopita baada ya kutangaza faida halisi ya shilingi milioni 513 (takriban dola za kimarekani milioni 3.98) katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.