Katika hali inayotia wasiwasi ya uvunjaji sheria katika Kaunti ya Murang’a, mamia ya wakazi wenye hasira wa kijiji cha Karung’e huko Mathioya, Jumapili jioni walivamia kituo cha polisi na kambi ya chifu, na kuwafanya maafisa waliokuwa na silaha wakimbie.
Wakaazi hao walisema walipata fununu kuhusu mshukiwa wa mauaji anayezuiliwa katika kituo cha polisi cha kushika doria cha Karung’e.
Vijana hao waliotaka kumuua mshukiwa huyo aliyewekwa rumande, walivamia na kuondoka tu baada ya kuthibitisha kuwa hakuzuiliwa hapo.
Agosti 4, 2024, mkazi mmoja aliyejulikana kama Bw Jamleck Irungu, mchuuzi wa mbao, alivamiwa alipokuwa akitoka katika baa ya eneo hilo.