Namibia imetoa wito wa kuongeza ufadhili wa ndani na uratibu bora wa mipango ya afya ili kuendeleza juhudi za kudhibiti UKIMWI wakati wa kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kupungua kwa msaada wa kimataifa.
Waziri wa afya na huduma za kijamii wa nchi hiyo Bw. Kalumbi Shangula, jana mjini Windhoek kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa mtandao wa Kiufundi wa Kikanda alisisitiza uboreshaji wa rasilimali za kudhibiti UKIMWI wakati changamoto zinaendelea, hasa kutokana na kupungua kwa fedha za kimataifa na athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga la COVID-19.
Amesisitiza haja ya kuongeza uungaji mkono wa kifedha wa kitaifa na uratibu bora zaidi wa mipango ya afya ili kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI.