Kampuni ya Huawei ya China yaanzisha mafunzo ya usalama wa mtandao wa Internet kwa maofisa wa Zimbabwe
2024-08-20 09:34:10| CRI

Kampuni ya teknolojia ya China Huawei imeanzisha mradi wa kwanza wa mafunzo ya usalama wa mtandao wa internet kwa maofisa wa serikali ya Zimbabwe mjini Harare, ili kuwasaidia kupambana na matishio ya mtandao wa internet.

Maofisa 100 kutoka wizara na idara za serikali wameshiriki kwenye mradi huo wa mafunzo ya siku nne, ulioandaliwa na Huawei ikishirikiana na wizara ya Tehama, huduma za Posta na Usafirishaji wa Vifurushi.

Mada za mafunzo hayo ni pamoja na mwelekeo wa usalama wa mtandao wa internet wa kimataifa, vigezo vya usalama vya kimataifa, usimamizi wa ulinzi binafsi wa kampuni, na usimamizi wa usalama wa data za kampuni.