Takwimu mpya zilizotolewa na Kituo cha uwekezaji cha Tanzania TIC, zinaonesha kuwa Tanzania imerekodi miradi 490 yenye thamani ya dola bilioni 4 za kimarekani katika miezi ya saba ya mwanzo ya mwaka huu, huku China ikiongoza.
TIC imesema kati ya miradi 490, miradi ya kilimo inaongoza na kutoa nafasi za ajira 163,356 kwa ujumla, ikilinganishwa na miradi 267 yenye thamani ya dola bilioni 2.6 za kimarekani iliyotoa nafasi 39, 230 za ajira.
Kituo hicho kimesema miradi hiyo inahusiana na sekta za kilimo, ujenzi wa majengo ya kibiashara, nishati, miundombinu ya kiuchumi, mashirika ya kifedha, rasilimali watu, viwanda, madini na petroli, huduma, mawasiliano ya simu, utalii na uchukuzi.
TIC pia imesema China inaendelea kuongoza kati ya nchi 10 za kigeni zinazowekeza zaidi kutoka mwaka 1997 hadi 2024, ikiwa na miradi 1,360 yenye thamani ya dola bilioni 11.5 za kimarekani na kutoa nafasi 155, 596 za ajira.