Rais Xi Jinping wa China amesema China itaendelea kuunga mkono Bunge la Umma la China (NPC) katika kuimarisha ushirikiano na Umoja wa mabunge duniani (IPU).
Rais Xi alisema hayo alipokutana na viongozi wa mabunge ya kigeni waliohudhuria maadhimisho ya miaka 40 ya bunge la Umma la China kujiunga na IPU, pamoja na semina ya kikanda ya mwaka 2024 kuhusu mafanikio ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa mabunge ya nchi zinazoendelea mjini Beijing.
Rais Xi amekaribisha ziara ya maspika nchini China, akibainisha kuwa wanatoka nchi za mabara tofauti, lakini wote ni wanachama wa nchi za kusini, na kwamba licha ya kuwa na hali tofauti za kitaifa, China na nchi hizi zote ni ndugu na washirika wazuri wenye maono ya pamoja.