Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema dola za kimarekani milioni 28.6 zimetengwa kwa ajili ya mwitikio wa kibinadamu nchini Somalia.
Kwa mujibu wa OCHA fedha hizi zilizotolewa na Mfuko wa Kibinadamu wa Somalia (SHF), zinalenga hatua za uingiliaji za kuokoa maisha kwenye maeneo yasiyofikika kirahisi na yanayokosa huduma za kimsingi.
Fedha hizo zimewawezesha washirika 54 wa kibinadamu kutoa misaada ya haraka kwenye mafuriko yaliyotabiriwa, ukame mkali na kuimarisha usalama na uratibu.
OCHA imesema, ujumuishwaji wa wanawake, wasichana na watu wenye ulemavu unahakikishwa katika maeneo yote, na asilimia 90 ya miradi inachangia usawa wa kijinsia kwa njia mbalimbali.