Mkutano wa kilele wa FOCAC kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Afrika
2024-08-21 09:53:08| CRI

Mkuu wa ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika Bw. Hu Changchun amesema, mkutano wa kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) unaotarajiwa kufanyika mwezi Septemba mjini Beijing, utatia nguvu katika uhusiano kati ya China na Afrika, kuendeleza kwa pamoja juhudi za kujijenga kuwa za kisasa na kuhimiza ujenzi wa  jumuiya ya ngazi ya juu kati ya China na Afrika yenye mustakbali wa pamoja.

Bw. Hu amesema hayo katika mkutano na wanahabari kuhusu mkutano mkuu wa tatu wa kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC 2024, huku akisema mkutano huo wa FOCAC utakaofanyika unatarajiwa kuzidi kuimarisha mshikamano na ushirikiano kati ya China na Afrika. Pia amesema mkutano huo utatoa mchango katika kuhimiza usasa wa kimataifa na ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

Ameongeza kuwa mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC wa mwaka 2024 utakuwa shughuli ya kusherehekea urafiki kati ya China na Afrika, kutafuta ushirikiano na kupanga mpango wa siku za baadaye chini ya kaulimbiu ya “Kushikana mkono katika kuhimiza usasa na kujenga jumuiya ya ngazi ya juu yenye mustakbali wa pamoja.”