Rais Xi Jinping wa China jana aliwapongeza wachezaji wa China walioshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris kwa uhodari wao na moyo wao wa michezo, akisema wameiletea heshima nchi yao na wananchi wake.
Alipokutana na ujumbe wa Olimpiki wa China, rais Xi amewahimiza wachezaji hao waendelee na juhudi na kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi kimichezo.