Waziri wa Ulinzi wa Israel Bw. Yoav Gallant amesema tawi la Rafah la kundi la Hamas limeshindwa na kuashiria kwamba wanajeshi wameanza kuelekeza nguvu zao kwenye mapigano dhidi ya kundi la Hezbollah kwenye mpaka wa Israel na Lebanon.
Bw. Gallant amesema hayo wakati wa ziara kwenye ushoroba wa Philadelphi, eneo linalodhibitiwa na Israel kwenye mpaka wa Gaza na Misri.
Wizara ya Ulinzi ya Israel ilitoa picha ya Bw. Gallan, akiwa amevalia fulana ya kuzuia risasi akizungukwa na makamanda, katika jengo la Palestina lililotekwa na wanajeshi wa Israel na kuligeuza kuwa makao makuu.
Amesema divisheni ya 162 ya jeshi la Israel imekishinda kikundi cha Rafah cha Kundi la Hamas, na wakati wa shambulizi, jeshi la Israel limeharibu mahandaki 150.