Kenya na China jana zimesaini makubaliano kuhimiza ushirikiano wa nishati mbadala katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Kaimu ofisa mkuu mtendaji katika Shirikisho la Nishati Mbadala la Kenya Bi. Cynthia Muhati, amesema chini ya ushirikiano huo, China inatarajiwa kuisaidia Kenya kukusanya mitaji kwa ajili ya uwekezaji wa ziada katika miradi ya nishati ya kijani.
Bi. Muhati amesema hayo huko Nairobi, wakati wa mkutano wa ujumuishwaji wa kifedha wa kidijitali kati ya China na Afrika mwaka 2024, huku akiongeza kuwa Kenya pia itanufaika na ujenzi wa uwezo kwa kupitia teknolojia kutoka China, ili kuhakikisha wakazi wa huko wanaendeleza teknolojia za nishati ya jua na nishati nyingine mbadala na bidhaa zenye ushindani.
Mkutano huo wa siku moja uliohudhuriwa na washiriki 100 kutoka China na Afrika, ulilenga kujadili mikakati ya kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha.