IOM laomba dola za kimarekani milioni 18.5 kuwasaidia wahamiaji walioathiriwa na Mpox
2024-08-22 08:52:50| CRI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeomba ufadhili wa dola za kimarekani milioni 18.5 kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa watu walioathiriwa na mlipuko wa homa ya Mpox katika maeneo ya mashariki, pembe ya Afrika na kusini mwa Afrika, wakiwemo watu waliopoteza makazi.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bi. Amy Pope amesema maambukizi ya Mpox yameleta wasiwasi mkubwa haswa kwa jamii kubwa ya wahamiaji na kwenye makazi ya wakimbizi ambayo hupuuzwa katika mazingira magumu. Kwa mujibu wa shirika hilo, ufadhili huo unatarajiwa kutumika kwa kuimarisha uwezo wa kukidhi mahitaji ya jamii hiyo kupitia hatua za kukinga na kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo, hasa katika maeneo ya mipakani.