Maonyesho ya tano ya vipindi vya tamthilia ya “Mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Afrika” yafunguliwa mjini Cairo
2024-08-22 10:22:29| cri

Awamu ya tano ya shughuli ya “Mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Afrika” ambayo ni maonyesho ya vipindi vya filamu na tamthilia za China yamefunguliwa rasmi tarehe 20 Agosti mjini Cairo nchini Misri.

Vipindi zaidi ya 20 vya filamu na tamthilia za China zinazotafsiriwa kwa lugha saba ikiwa ni pamoja na Kiingereza, Kifaransa na Kiarabu zitaonyeshwa kupitia vyombo vya habari zaidi ya 20 katika nchi 15 za Afrika. Maonyesho hayo yaliandaliwa pamoja na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na vyombo vya habari vya nchi nyingi za Afrika, ikiwa ni pamoja na Misri, Kenya, Tanzania, Ethiopia, Burundi na kadhalika. Vipindi vya filamu na tamthilia za China zinazotafsiriwa kwa lugha za Kifulani na Kiamharic vitaonyeshwa kwa mara ya kwanza barani Afrika.

Tangu mwaka 2021, CMG imefanya maonyesho manne ya “Mawasiliano ya kirafiki kati ya China na Afrika”, shughuli ambayo vipindi zaidi ya 120 vya filamu na tamthilia za China vimeonyeshwa kwa watazamaji takriban milioni 500 wa Afrika kwa ujumla.