Mahakama ya Kenya imezindua mkakati elekezi ili kutetea ujumuishaji wa uendelevu wa mazingira katika mfumo wa haki nchini Kenya.
Jaji mkuu wa Kenya Bibi Martha Koome amesema mahakama imejitolea kutetea uendelevu wa mazingira kwenye makahama nchini Kenya, kupitia kufuata sheria, kulinda haki za kuhakikisha maendeleo endelevu, na kuhimiza udumishaji wa ikolojia.
Akiongea mjini Nairobi kwenye uzinduzi wa mfumo huo, Bibi Koome amesema kwa kupitia mfumo huo, mahakama ya Kenya inathibitisha kujumuisha uendelevu wa mazingira katika utendaji wa mahakama za Kenya. Jaji mkuu pia amebainisha kuwa mahakama ya Kenya inaweka vigezo vya juu na kuwa mfano wa kufuatwa na sekta nyingine.