Rais Xi Jinping wa China Jumanne alikutana na ujumbe wa wanamichezo wa China walioshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing.
Rais Xi amesisitiza kuwa katika michezo ya Olimpiki, wanamichezo wa China walishikamana na kushindana kwa ushupavu kuelekea ubingwa, na kupata matokeo mazuri zaidi katika historia ya ushiriki wa China kwenye Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto katika nchi ya nje. Mafanikio yao ni ushindi kwenye matokeo ya mashindano na vilevile katika moyo wa uanamichezo, wakileta heshima kwa taifa na wananchi.
Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali, Rais Xi alikaribisha ujumbe huo nyumbani, kuwapa pongezi wanamichezo wa ujumbe huo, na kutoa salamu kwa makomredi wote wa sekta ya michezo nchini kote.