China yatoa msaada wa chakula kwa Zimbabwe kutokana na ukame unaosababishwa na El Nino
2024-08-23 08:32:18| CRI

China imetoa msaada wa chakula cha dharura kwa Zimbabwe ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na uhaba mkubwa wa chakula uliotokana na ukame unaosababishwa na athari za El Nino.

Balozi wa China nchini Zimbabwe Bw. Zhou Ding amekabidhi tani 1,760 za mchele kwa Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Harare, na kuhudhruiwa na mawaziri, maofisa waandamizi, na wawakilishi wa taasisi zitakazopokea msaada huo.

Rais Mnangagwa ameishukuru serikali ya China kwa msaada huo, na kusema China imekuwa ikiisaidia Zimbabwe kila inapokabiliwa na tatizo hili la uhaba wa chakula. Amesema msaada huo utagawiwa kwa wanajamii walio hatarini zaidi, ikiwa ni pamoja na vituo vya watoto yatima, taasisi zinazohudumia wazee na watu wenye ulemavu.