Xi Jinping kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa FOCAC wa mwaka 2024
2024-08-23 10:38:50| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying leo ametangaza kuwa Rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC wa mwaka 2024 tarehe 5, Septemba. Katika kipindi cha Mkutano huo wa kilele, Rais Xi pia atafanya tafrija ya kuwakaribisha viongozi wa nchi za Afrika, mashirika ya kikanda na kimataifa walioalikwa kuhudhuria Mkutano huo na kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za pande mbili mbili.