Hafla ya kuwaaga wanafunzi wa Kenya waliopata udhamini wa masomo wa serikali ya China yafanyika Nairobi
2024-08-23 08:33:02| CRI

Shughuli ya kuwaaga wanafunzi wa Kenya waliopata udhamini wa masomo kutoka kwa serikali ya China kwa ajili ya kuendelea na masomo ya juu katika vyuo vikuu nchini China, imefanyika kwenye ubalozi wa China nchini Kenya.

Shughuli ya kuwaaga wanafunzi 13 walionufaika na udhamini huo, iliambatana na hafla ya kuwapatia tuzo washindi wa Shindano la Insha la "China-Africa Cooperation in My Eyes".

Maofisa waandamizi wa Kenya, wanadiplomasia, wanafunzi, wazazi, na walimu walihudhuria hafla hiyo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ya Kenya Bibi Beatrice Inyangala, alipongeza ushirikiano imara kati ya Kenya na China katika sekta ya elimu ya juu na kuwapa ujuzi vijana wa Kenya.