Kura ya maoni ya CGTN | Mchezo "Wukong" wafurika kwenye skrini, "mchezo+utamaduni" kuchochea shauku ya wachezaji duniani
2024-08-23 14:33:15| cri

Mchezo wa ngazi ya AAA uliotengenezwa na China, ujulikanao kama Wukong unaunda "hadithi" mpya! Mchezo huu wa kompyuta, uliowekwa kwenye msingi wa hadithi za Kichina, umefika kilele cha chati ya Michezo ya Kompyuta Iliyochezwa Zaidi ya Steam ndani ya saa moja baada ya kuzinduliwa, na kupata pongezi nyingi kutoka kwa wachezaji kote ulimwenguni.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na CGTN katika dunia nzima, wahojiwa wengi wanaamini kwamba mchezo huu unaonesha nguvu ya sekta ya michezo ya kompyuta ya China na kuchochea hamu yao ya kupenda utamaduni wa jadi wa China.

Umaarufu wa mchezo wa Wukong unatokana na kiwango chake bora cha utengenezaji wa mchezo. IGN China, chombo kikuu cha michezo ya kompyuta na habari za burudani duniani, kiliupa mchezo huu alama bora, na kuuita hatua muhimu katika tasnia ya michezo ya kwenye kompyuta ya China na michezo inayozalishwa nchini yenye ushindani mkubwa katika soko la kimataifa.

Katika utafiti huo, asilimia 88.2 ya wahojiwa waliamini kuwa mchezo huu unawakilisha ubora wa juu wa utengenezaji wa aina hii ya michezo ya kompyuta nchini China, ukionesha uwezo mkubwa wa tasnia ya michezo ya ya kompyuta nchini China. Mwanamtandao mmoja alitoa maoni akisema, "Sichezi michezo ya video lakini nimeona michoro (ya mchezo Wukong) ya kushangaza sana.