Umoja wa Ulaya yatangaza sera mpya ya kutoza ushuru kwa magari ya umeme ya China
2024-08-23 14:32:41| cri

Kamati ya Umoja wa Ulaya tarehe 20 Agosti mwaka 2024, ilitoa uamuzi wa mwisho wa uchunguzi dhidi ya magari ya umeme ya China AS689, ikitangaza kutoza ushuru wa 17%-36.3% kwa kampuni za China. Kesi hiyo ilitangazwa na rais wa Kamati ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen wakati alipotoa ripoti kuhusu Hali ya Umoja wa Ulaya tarehe 13 Septemba mwaka 2023, kwa lengo la kuweka nafasi kwa ajili ya mabadiliko na maendeleo ya sekta ya magari ya umeme ya Umoja huo, na kuanzishwa rasmi na Kamati ya Umoja wa Ulaya tarehe 4 Oktoba mwaka huo huo. Nchi wanachama mbalimbali wa Umoja wa Ulaya, wadau kutoka sekta ya magari pamoja na washauri bingwa na wasomi wanaona kuwa, hii ni hatua ya kujilinda kibiashara kwa kisingizio cha kujidai kulinda “biashara ya haki”, na kwamba maendeleo ya magari ya umeme ya Umoja wa Ulaya hayapaswi kuogopa kukabiliana na ushindani.