Maofisa na wasomi wa Afrika washiriki kwenye mafunzo kuhusu mandhari ya miji nchini China
2024-08-23 10:01:31| CRI

Maofisa na wasomi 18 kutoka nchi sita za Afrika wanashiriki kwenye mafunzo kuhusu upangaji na ujenzi wa mandhari za miji nchini China.

Mafunzo ya siku 14 yalianza jumatano mjini Hangzhou, mkoani Zhejiang yamewaleta pamoja washiriki kutoka Misri, Ethiopia, Nigeria, Mauritius, Lesotho na Tunisia, ambao watapata mafunzo yao mjini Hangzhou, Guiyang na sehemu nyingine.

Mafunzo hayo yameandaliwa na wizara ya biashara ya China na kituo cha utafiti wa mianzi cha China, ambacho ni sehemu ya mamlaka ya taifa ya misitu na mbuga za majani.

Naibu mkuu wa Kituo cha utafiti wa mianzi cha taifa cha China Bw. Wu Tonggui, amesema mradi huo utatoa mapendekezo ya marejeleo kwa nchi za Afrika kuhusu jinsi ya kulinda na kutumia maliasili kujenga mandhari ya kipekee katika miji yao.