Serikali mpya ya Afrika Kusini yaendeleza urafiki kati yake na China
2024-08-23 10:02:32| CRI

Naibu rais wa Afrika Kusini Bw. Paul Mashatile amesema serikali mpya ya Afrika Kusini itaendelea kufuata kithabiti sera za kirafiki kwa China na inapenda kupanua ushirikiano na China, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo makubwa zaidi.

Bw. Mashatile amesema hayo mjini Pretoria wakati akipokea hati za utambulisho kutoka kwa balozi mpya wa China nchini Afrika Kusini Bw. Wu Peng, na kuishukuru China kwa msaada wake muhimu wa muda mrefu kwa maendeleo ya Afrika Kusini.

Bw. Wu Peng amesema uhusiano kati ya China na Afrika Kusini umeingia katika "kipindi cha dhahabu", na kwamba kudumisha na kuendeleza uhusiano huo si tu kwamba kunalingana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili, bali pia kutaingiza nguvu mpya kwenye amani na utulivu wa dunia.