Katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja ya amani na usalama unaendelea kwa kasi. Kuanzia Mkutano wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2012, China ilipozindua kwa mara ya kwanza Mpango wa Wenzi wa Ushirikiano wa Amani na Ushirikiano kati ya China na Afrika”, ikiorodhesha rasmi ushirikiano wa amani na usalama katika mipango muhimu ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, hadi “Ujenzi wa Amani na Usalama” uliowekwa katika “Miradi Tisa” ambayo ilitolewa katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa FOCAC, China imekuwa ikichangia zaidi mambo ya usalama wa Afrika kwa msingi wa kuheshimu kikamilifu matakwa ya nchi za Afrika na kufuata kanuni za kimsingi za mahusiano ya kimataifa.
Katika mambo ya ulinzi wa amani duniani, zaidi ya asilimia 80 ya walinda amani wa China wanapelekwa barani Afrika ikiwa na zaidi ya 32,000. Na China ni nchi inayopeleka idadi kubwa zaidi ya walinda amani barani Afrika kati ya nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Katika operesheni hizo za kulinda amani, wanajeshi wanawake wanashika nafasi muhimu. Katika miaka mingi iliyopita, China imetuma askari wanawake zaidi ya 1,000 kushiriki katika operesheni za kulinda amani. Hadi leo, wanajeshi hao wanawake wanaonesha umuhimu mkubwa katika shughuli mbalimbali za kulinda amani za Umoja wa Mataifa, zikiwemo kukuza usawa wa kijinsia, kulinda haki na maslahi ya wanawake, na hata katika kuzuia migogoro na kuhimiza maendeleo ya amani. Askari mwanamke wa China Zhang Qin ni mmoja wao. Askari huyo akiwa askari wa kundi la tatu la China la kulinda amani nchini Sudan (Juba) alitunukiwa Tuzo ya Heshima ya Amani na Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa. Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tutaelezea hadithi ya Bibi Zhang Qin na wanawake wengine ambao wametoa michango muhimu katika kulinda amani duniani.