KNUT yaondoa tangazo la mgomo wa walimu
2024-08-26 23:03:04| cri

Chama cha Walimu nchini Kenya (KNUT) kimewataka walimu wafike sehemu zao za kazi kwa masomo ya muhula wa tatu leo hii baada ya kufuta mgomo uliokuwa uanze hii leo.

Mgomo wa walimu nchini Kenya ulipangwa kuanza leo baada ya vyama vya walimu kutoa tangazo la mgomo wa kitaifa na kuwataka walimu kutokwenda kazini hadi matakwa yao yote yatakaposhughulikiwa na serikali.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa KNUT Collins Oyuu amesema, madai ya walimu yanashughulikiwa kiutawala.

Wakati huohuo, Chama cha walimu wa shule za upili na vyuo (KUPPET) kimetangaza kuendelea na mgomo wa walimu kuanzia leo Jumatatu kama ilivyopangwa awali.