Rais wa Zanzibar awashukuru wataalamu wa afya wa China kwa juhudi za kutokomeza ugonjwa wa kichocho
2024-08-27 09:50:41| CRI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Hussein Ali Mwinyi Jumatatu aliishukuru timu ya madaktari wa China kwa mchango wao katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa kichocho visiwani Zanzibar.

Akizungumza na wataalamu hao wa afya kutoka China katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika Ikulu Zanzibar baada ya kumalizika kwa mradi wa kuzuia na kudhibiti ugonjwa wa kichocho unaofadhiliwa na China kisiwani Zanzibar, Dkt Mwinyi alisema mradi huo umesaidia makundi yaliyo katika mazingira hatarishi katika visiwa hivyo.

Alibainisha kuwa mradi huo pia uliboresha mfumo wa kinga na udhibiti wa magonjwa Zanzibar na utaongeza zaidi urafiki kati ya China na Zanzibar. Dkt Mwinyi pia aliishukuru China kwa msaada wake wa kujitolea kwa Zanzibar katika sekta ya matibabu na afya ya umma kwa miaka mingi.

Naye kiongozi wa timu ya madaktari wa China, Huang Yuzheng alisema anatarajia kupata msaada mkubwa kutoka kwa serikali ya Zanzibar katika utekelezaji wa mradi ujao.