Mkutano wa 74 wa Kamati ya kanda ya WHO Afrika wafunguliwa nchini Jamhuri ya Kongo
2024-08-27 22:33:58| cri

Mkutano wa 74 wa Kamati ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika umefunguliwa jana jumatatu katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo, Brazzaville.

Akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo, rais wa Jamhuri ya Kongo Denis Sassou Nguesso ametoa wito kwa nchi za Afrika kuunda muungano utakaounga mkono pendekezo la “Ubora katika Huduma za Msingi za Afya.”

Mkutano huo unaofanyika kuanzia jana na unatarajiwa kumalizika ijumaa wiki hii, unahudhuriwa na washiriki 1,000 akiwemo Katibu Mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus na mawaziri wa afya kutoka nchi 47 wanachama wa Afrika ambao wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya kiafya yanayolihusu bara la Afrika.