Shirika la Afya Duniani (WHO) Jumatatu lilianzisha harakati za kimataifa za kukabiliana na maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu.
Mpango Mkakati wa Maandalizi na Mwitikio utaanza Septemba 2024 hadi Februari 2025, na kuhitaji dola za Kimarekani milioni 135. Kwa kuratibu juhudi za kimataifa, kikanda na kitaifa, mpango huo unalenga kuimarisha mikakati ya ufuatiliaji na mwitikio, kuhakikisha upatikanaji sawa wa uchunguzi na chanjo, kupunguza maambukizi kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu, na kuziwezesha jamii kudhibiti milipuko.
Mpango wa chanjo unalenga wale walio katika hatari zaidi, kama vile watu wanaowasiliana kwa karibu na wagonjwa na wafanyakazi wa afya, na kuvunja minyororo ya maambukizi. Pia utalenga kutoa uongozi wa kimkakati na mwongozo, na kuhakikisha upatikanaji wa matibabu kwa makundi yaliyo hatarini katika maeneo yaliyoathirika.
Kwa mujibu wa taarifa ya WHO, maombi ya ufadhili yatazinduliwa hivi karibuni.