Mkutano wa Mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafanyika mjini Beijing, China kuanzia Septemba 4 hadi 6.
Mchumi wa zamani katika Benki ya Dunia ambaye pia ni mshauri wa serikali ya Kenya Dkt. Mwangi Wachira amesema, China ni mwenzi wa Afrika katika njia ya kutimiza mambo ya kisasa, na ushirikiano kati yao unatoa fursa za kimkakati kwa pande hizo mbili kushirikiana kukuza viwanda na kujiendeleza kwa kasi.
Katika mazungumzo ya viongozi wa China na Afrika ya mwaka jana, Rais wa China Xi Jinping alitangaza mipango mitatu kuhusu Afrika, ambayo ni Mpango wa kusaidia maendeleo ya viwanda ya Afrika, Mpango wa China wa Uboreshaji wa Kilimo cha kisasa wa Afrika, na Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa kuwaandaa wataalamu. Mipango hii inakidhi mahitaji ya maendeleo ya kisasa ya Afrika, kusaidia Afrika kujiendeleza uwezo wake, kuhimiza ujenzi wa maingiliano ya kikanda na mambo ya kisasa barani Afrika, na kuimarisha zaidi ushirikano wenye ufanisi kati ya pande hizo mbili.
Akizungumzia mipango hiyo, Dkt. Wachira anasema China ni mwenzi wa kimkakati wa Afrika katika mchakato wa kutimiza maendeleo ya mambo ya kisasa barani Afrika. Anasema Afrika inajitahidi kutumia fursa ya mapinduzi ya nne ya viwanda kupata maendeleo ya kuvuka nyakati, lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na msingi wake wa viwanda na teknolojia. Amesema China ikiwa mwenzi mkubwa katika mchakato wa Afrika wa kutafuta maendeleo ya kasi, sera na mipango yake mingi ya maendeleo inaendana na malengo ya Afrika, hali ambayo imeleta maendeleo ya haraka ya ushirikiano kati ya China na Afrika.
Dkt. Wachira anaona kuwa mzizi wa uhusiano mzuri na urafiki kati ya China na Afrika upo katika ukweli kwamba, pande hizo mbili siku zote ni wenzi katika njia ya kujiendeleza, na kwamba Wachina wako tayari kushirikiana na Afrika bila ya masharti yoyote ya thamani ya kimtazamo, na China inaisaidia Afrika kuwa ya kisasa kwa njia inayoendana na matakwa halisi ya Waafrika.