Wizara ya Afya nchini Sudan imesema, idadi ya watu waliofariki kutokana na mvua kubwa inayonyesha katika mikoa 10 nchini humo imefikia 138.
Ofisi ya Mambo ya Dharura iliyo chini ya Wizara hiyo imesema katika taarifa yake iliyotolewa jana kuwa, familia 31,666 zenye watu zaidi ya 129,650 zimeathiriwa na mvua hizo, na kuongeza kuwa nyumba 12,420 zimebomoka.
Wakati huohuo, Sudan imerekodi kesi mpya 102 na vifo vitano vinavyotokana na kipindupindu katika mikoa mitano, na kufanya jumla ya kesi za maambukizi kufikia 1,223 na vifo 48.