Mkutano wa Viongozi wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024 ambao ni muhimu kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili, utafanyika kuanzia Septemba 4 hadi 6 nchini China.
Akizungumzia jukwaa hilo, Msomi wa Somalia Bw. Abdilahi Ismail Abdilahi amesema, FOCAC ni jukwaa muhimu zaidi kwa China na Afrika kufanya mawasiliano, kutokana na kwamba China ni mfano mzuri wa kuigwa kwa nchi zinazoendelea, na Afrika ni sehemu muhimu katika maendeleo ya dunia, na maendeleo yake yataathiri mwelekeo wa dunia.
Katika mahojiano na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), Bw. Ismail amesema, akiwa Mwafrika, anatumai kuwa mkutano huo utaleta maendeleo na mabadiliko mengi zaidi kwa Afrika. Amesema anatumaini kuwa, kupitia mkutano huo, Somalia itafungua ukurasa mpya wa maendeleo na kuongeza ushirikiano na China katika sekta nyingi zaidi zikiwemo uchumi, biashara na usalama.