China yatoa waraka mweupe kuhusu mageuzi ya nishati
2024-08-29 14:59:23| cri

Idara ya Taifa ya Nishati ya China leo Alhamisi imetoa waraka mweupe kuhusu maguezi ya nishati. Waraka huo umeonesha kuwa, maendeleo ya nishati safi nchini China yamepiga hatua mpya kwa kufuata njia ya mageuzi inayoendana na hali halisi ya nchi na mahitaji ya zama za sasa.

Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2023, uwezo wa jumla wa mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo na jua nchini China umeongezeka kwa mara kumi kuliko miaka kumi iliyopita, na uzalishaji wa nyongeza wa umeme kwa nishati safi umechukua zaidi ya nusu ya matumizi ya nyongeza ya umeme nchini kote, huku matumizi ya nishati safi yakifikia asmilia 26.4 ya matumizi ya jumla ya nishati nchini China.