Mlipuko wa Mpox watishia soko la nje la Kenya
2024-08-29 23:07:32| cri

Mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya Nyani (Mpox) katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), unatishia soko la nje la Kenya linalokua kwa kasi zaidi ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), huku serikali ya nchi hiyo ikiimarisha uchunguzi ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo hatari nchini humo.

Mauzo ya bidhaa za Kenya nchini DRC, ambalo ni soko kuu la nje la wafanyabiashara wengi wa Kenya ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, yanakabiliwa na mkanganyiko mpya kufuatia uamuzi wa baadhi ya nchi zinazopakana na DRC kuweka vikwazo vikali vya afya ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo wa kutisha.

Kulingana na Shirika la Takwimu la Kenya (KNBS), katika robo ya kwanza ya 2024, mauzo ya Kenya hadi DRC yaliongezeka kwa zaidi ya nusu na kufikia Sh8.62 bilioni katika miezi mitatu ya kwanza ya mwaka.