Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amesema, kuunga mkono maendeleo ya Afrika ni wajibu wa pamoja wa jamii ya kimataifa, na China iko tayari kushirikiana na jamii ya kimataifa kuimarisha ustawi wa Afrika na kuleta manufaa kwa watu wa Afrika.
Lin Jian amesema hayo jana katika mkutano na wanahabari ikiwa ni majibu ya kauli iliyotolewa na mchumi wa Kenya kuhusu ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema nchi za Afrika hazilazimishwi kubadilisha sera zao, na ushirikiano wa China na Afrika unachochewa na mahitaji ya nchi za Afrika.
Lin Jian amesema, ushirikiano huo, ambao msingi wake ni maslahi ya watu wa China na Afrika, daima umekuwa ukiongozwa na kanuni ya uaminifu, matokeo halisi, uhusiano mwema na nia nzuri.