China yatoa ripoti kuhusu “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
2024-08-29 15:01:24| cri

Kamati Kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China leo imetoa ripoti ya mwaka 2024 kuhusu maendeleo ya ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Ripoti hiyo inaonesha kuwa hadi sasa nchi 52 za Afrika na Umoja wa Afrika zimesaini makubaliano na China kuhusu ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Pia ripoti hiyo imesema, mashirika ya China yamejenga au kukarabati zaidi ya kilomita elfu 10 za reli, kilomita 100,000 za barabara, kujenga madaraja karibu 1,000, bandari 100, mtandao wa umeme takriban kilomita 66,000 na mtandao wa mawasiliano ya habari takriban kilomita laki 1.5.