Mazungumzo ya duru mpya ya kimkakati kati ya China na Marekani yafanyika Beijing
2024-08-29 09:12:14| CRI

Mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya nje ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC Bw. Wang Yi na mshauri wa usalama wa taifa wa Marekani Bw. Jake Sullivan walifanya mazungumzo ya dura mpya ya kimkakati kati ya China na Marekani jana hapa mjini Beijing.

Kwenye mazungumzo yao, Wang alisema kuanzishwa kwa maelewano ya pamoja yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili huko San Francisco ni kazi kuu ya mazungumzo hayo ya duru mpya.

Wang pia ameitaka Marekani kuacha kuikandamiza China katika masuala ya uchumi, biashara na teknolojia na kufuata ahadi yake ya kutounga mkono “Taiwan ijitenge na China”, na pia kuacha kuitupia jukumu China katika suala la Ukraine.

Mbali na hayo, Bw. Wang Yi na Bw. Jake Sullivan pia walijadili mazungumzo ya duru mpya kati ya marais wa nchi hizo mbili katika siku za usoni.