Rais Xi anasisitiza China, Afrika daima ni jumuiya yenye mustakbali wa pamoja
2024-08-30 21:18:24| cri

Rais wa China Xi Jinping amesema China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

Akijibu barua kwa wasomi kutoka nchi 50 za Afrika, Rais Xi amebainisha kuwa, kutokana na hali yenye utatanishi na iliyofungamana duniani, China na Afrika zinahitaji kuimarisha mshikamano na ushirikiano zaidi kuliko ulivyokuwa hapo awali.