Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Lin Jian amesema China iko tayari kuanza safari mpya na Afrika kuelekea usasa na kutoa mchango kwa pamoja katika usasa wa dunia na maendeleo ya pamoja ya binadamu.
Bw. Lin Jian ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari wakati alipojibu maoni ya wataalamu na wasomi wa Afrika kwamba China kwa ushirikiano wake na Afrika italifanya bara hilo liwe huru kufuata mtindo wa Afrika ya kisasa na pande hizo mbili zinatakiwa kushirikiana katika njia zao za kuleta maendeleo ya kisasa.
Akibainisha kuwa kutimiza usasa ni kazi ya pamoja ya China na nchi za Afrika, Lin alisema kuwa China inaunga mkono kithabiti Afrika katika kutafuta njia ya maendeleo ya kujitegemea na kutilia mkazo maeneo matatu ambapo usasa unahitajika zaidi wa Afrika.
Ameeleza kuwa walizindua Mpango wa Kusaidia Maendeleo ya Viwanda barani Afrika, na kutekeleza Mpango wa China Kusaidia Maendeleo ya Kilimo barani Afrika na Mpango wa Ushirikiano kati ya China na Afrika wa Maendeleo ya kuwaandaa watu chini ya mfumo wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ili kusaidia maendeleo ya Afrika na ustawi kwa hatua madhubuti.