Serikali ya Ethiopia inawahimiza wawekezaji wa China kutafuta fursa ndani ya maeneo ya viwanda nchini humo na eneo lake la kwanza la biashara huria.Wito huu ulitolewa na Fisseha Yitagesu, afisa mkuu mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Maeneo ya Viwanda la Ethiopia (IPDC), na maafisa wengine wakuu wa Ethiopia wakati wa mkutano wa hivi karibuni wa kukuza uwekezaji.Yitagesu alisema kuwa wawekezaji wa China kwa sasa wamekuwa wawekezaji wengi zaidi wa kigeni katika maeneo ya viwanda yanayosimamiwa na IPDC kote Ethiopia, akisisitiza umuhimu wa kuvutia makampuni zaidi ya viwanda ya China kwenye maeneo 13 ya viwanda nchini humo na Eneo la Biashara Huria la Dire Dawa.