Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema, watu 472,000 katika kaunti 78 nchini Sudan Kusini wameathiriwa na mafuriko ya ghafla yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini humo.
Katika ripoti yake iliyotolewa jana, OCHA imesema mafuriko hayo yaliyoanza mwezi Mei, yamesababisha uharibifu wa nyumba, mazao, kuvuruga mfumo wa elimu na afya, na watu kushindwa kupata huduma muhimu, na hivyo kuongeza hatari ya mlipuko wa magonjwa.
OCHA imeonya kuwa, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha pamoja na kumwagwa kwa maji kutoka Ziwa Victoria, kumeongeza kiwango cha maji cha Mto Nile, na hivyo kuathiri watu 472,000 nchini Sudan Kusini.